Thursday, September 2, 2010
Pakistan yawaacha 'watatu'
Meneja wa timu ya Pakistan Yawar Saeed amesema wachezaji watatu wa kriketi wa Pakistan wanaotuhumiwa kupanga matokeo hawatacheza michezo yete iliyosalia nchini Uingereza.
Butt, Asif na Amir wanaotuhumiwa kupanga matokeo
Salman Butt, Mohammad Asif na Mohammad Amir, wanachunguzwa na polisi kuhusiana na tuhuma kuwa Asif na Amir walirusha mipira mibovu kwa makusudi.
Mwenyekiti wa bodi ya kriketi ya Pakistan (PCB) Ijaz Butt alisema siku ya Jumatano kuwa wachezaji hao wanaweza kuendelea kucheza.
Lakini Saeed amesema "nimeamua kutowachezesha, na sio kwamba wamesimamishwa uchezaji".
Nahodha wa michuano ya test Salman Butt na warusha mipira Asif na Amir, wako mjini London wakiwa katika kikao cha uchunguzi cha PCB kuhusiana na matukio kwenye mchezo kati ya Pakistan na England kwenye uwanja wa Lords. Wachezaji wenzao wanacheza mchezo wa mazoezi dhidi ya Somerset huko Taunton.
Pakistan, ambao walipoteza mchezo wao wa Test kwa 3-1, watacheza tena michezo miwili ya Twenty20 dhidi ya England, wa kwanza ukifanyika Jumapili mjini Cardiff, kabla ya kucheza michezo mitano ya one-day series.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment