Tuesday, June 18, 2013
MASTAA wakubwa wenye mafanikio ya kasi mithili ya moto wa petroli
MASTAA wakubwa wenye mafanikio ya kasi mithili ya moto wa petroli, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ na Jacqueline Wolper Masawe, wanatajwa kuwa wafuasi wa imani ya jamii ya siri ya Freemasons, lakini swali zito limeibuka.
Diamond na Wolper, wote wameshakanusha kuwa Freemasons japo chini kwa chini inasisitizwa, ila swali kuu ni kuhusu kafara, ikidodoswa ni nani wamemuua ili kufanikiwa?
Zipo taarifa kuwa masharti ya Freemasons ni kumtoa mzazi au ndugu wa damu kafara ili ukubalike kwenye jamii yao na kumwagiwa mafanikio ya utajiri wa haraka.
Kutokana na maelezo hayo kuhusu kafara, swali linalogota ni kwamba kama ni kweli wao ni Freemasons na wanatakiwa kumtoa kafara mtu kama sadaka, mbona hawajawahi kuripotiwa kuwa na msiba wa ndugu au mzazi yeyote?
Mdau wa filamu, Jessica Marsha, alisema kuwa haamini kama Diamond na Wolper ni Freemasons kwa sababu hawajawahi kufiwa.
“Tena ninavyojua mimi ni kwamba ukiingia Freemasons, mtu wa kwanza kumtoa kafara ni mama mzazi, Diamond na Wolper kila mmoja ana mama yake ambaye yupo hai,” alisema Jessica na kuongeza:
“Wale wana mafanikio binafsi. Diamond anafanikiwa kwa kipaji chake cha muziki, Wolper yeye ni juhudi zake kwenye filamu na nyongeza kubwa anayopata kupitia kwa mchumba wake Dallas ambaye ni tajiri sana.”
DIAMOND HAJUI KABISA
Kilichofanya watu wengi wakapaza sauti kwamba Diamond ni Freemason ni picha ambayo alipiga na jamaa wa Kizungu nchini Uingereza.
Picha hiyo, ukitazama mavazi meusi ambayo Diamond alishabihiana na jamaa huyo pamoja na ishara ya vidole waliyoonesha, vipo kwenye mrengo wa Freemasons.
Hata hivyo, Diamond anakanusha kuwa Freemasons na anadai jamaa huyo wa Kizungu alimlazimisha. Diamond: “Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha.
“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu, nikampa ushirikiano alioutaka. Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemasons. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua lakini mimi siyo Freemasons.”
WOLPER AKIRI KUFUATWA
Katika maelezo yake, Wolper alisema kuwa anahisi watu wanasema yeye ni Freemasons kwa sababu ya mavazi yake, kwani baadhi ya watu husema yana alama za imani hiyo.
Kuhusu yeye anavyojitambua, akasema: “Mimi siyo Freemasons, nakumbuka kuna siku watu walinifuata wakaniambia nijiunge Freemasons nitakuwa na mafanikio lakini sijakubaliana nao.”
ELIMU YA KAFARA
Mtaalamu wa nyota, aliye na elimu kubwa kuhusu jamii za siri, ikiwemo Freemasons, Maalim Hassan Yahya Hussein alisema kuwa msingi halisi wa Freemasons ni kutoa kafara lakini siyo lazima binadamu.
Maalim Hassan alisema: “Mara nyingi hufanya kafara ya mnyama hasa mbuzi na kondoo. Anaweza kuwa hata ng’ombe mwenye pembe zilizochongoka ambazo hutengeneza ile alama ya vidole viwili katika salamu za Freemasons.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment