Thursday, May 27, 2010

Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome


Jahazi wanasema:

Malipo ni duniani, akhera kuhesabiwa
usijigeuze nyani, kucheka uliyoombewa,
wajua unakotoka, hujui unakokwenda
mithili ya rabuka, haijui mwanamwenda
hata uwe unaruka, kwa mola huwezi kwenda
-
Alopewa mitihani, mungu hajamuonea
Msikae vikaoni, vidole kumnyooshea

--
Kibwagizo
-----------

Wasafirishe wapeleke pwani na jahazi
Mwanamke nyonga, makalio ni majaliwa
Uongo Uongo?

Mrembo Mpya wa IFM Apatikana

Katika mashindano hayo ambayo yaliambatana na burudani ya nguvu toka kwa wasanii mbalimbali, warembo 11 ambao ni wanafunzi wa IFM walichuana kutafuta mrembo wa IFM kwa mwaka 2010.

Katika shindano hilo warembo watano waliibuka kuwa wawakilishi wa chuo hicho katika ngazi za juu za vyuo.

Warembo hao ni Flora Martin aliyeibuka Miss IFM mwaka 2010, Judith Osima alishika nafasi ya Pili na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Esther Emmanuel wakati nafasi ya nne ilichukuliwa na Editruda Msoka na ya tano ilinyakuliwa na Pendo Sam.

KATIKA shindano hilo mshindi wa kwanza Miss IFM Flora Martin aliibuka na zawadi ya Laptop yenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 na pesa taslimu shilingi 300,000, mshindi wa pili alizawadiwa Dressing table yenye thamani ya shilingi 500,000 na pesa tasilimu shilingi 200,000.

Mshindi wa tatu aliibuka na TV aina ya Hitachi inchi 24, na kiasi cha shilingi 150,000.

Mshindi wa Nne na watano waliondoka na mshiko wa shilingi 120,000.

Jumla ya zawadi zote zilizoandaliwa katika shindano hili ziligharimu kiasi cha shilingi milioni 3.5.

Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia


Rima Fakih Mmarekani mwenye asili ya Lebanon amekuwa Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kushinda mashindano ya Miss USA katika historia ya mashindano hayo.

Katika mashindano yaliyofanyika mjini Las Vegas na kuonyeshwa live na televisheni ya NBC, Fakih aliwafunika jumla ya warembo 50 toka majimbo mbalimbali ya Marekani na kutwaa taji la Miss USA 2010.

Fakih mwenye umri wa miaka 24, alitwaa taji la urembo wa Marekani akifuatiwa na Miss Oklahoma aliyeshika nafasi ya pili, Miss Virginia, Miss Colorado na Miss Maine.

Fakih ataiwakilisha Marekani kwenye mashindano ya urembo ya Miss Universe yatakayofanyika baadae mwaka huu.

Burudani Time - Nyama ya Bata


Mhhh.. ni wakati mwingine wa burudani za mwisho wa wiki, tunawaletea Picha hii ya kundi la Offside Trick wakimshirikisha Mzee Yusuph wanauliza 'Je unakula bata we?'

NO PAIN NO GAIN

SALSA NI CHAGUO LETU

KARIBU NDANI YA MAISHANIENTERTAINMENT