Thursday, May 27, 2010
Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia
Rima Fakih Mmarekani mwenye asili ya Lebanon amekuwa Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kushinda mashindano ya Miss USA katika historia ya mashindano hayo.
Katika mashindano yaliyofanyika mjini Las Vegas na kuonyeshwa live na televisheni ya NBC, Fakih aliwafunika jumla ya warembo 50 toka majimbo mbalimbali ya Marekani na kutwaa taji la Miss USA 2010.
Fakih mwenye umri wa miaka 24, alitwaa taji la urembo wa Marekani akifuatiwa na Miss Oklahoma aliyeshika nafasi ya pili, Miss Virginia, Miss Colorado na Miss Maine.
Fakih ataiwakilisha Marekani kwenye mashindano ya urembo ya Miss Universe yatakayofanyika baadae mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment