Katika mashindano hayo ambayo yaliambatana na burudani ya nguvu toka kwa wasanii mbalimbali, warembo 11 ambao ni wanafunzi wa IFM walichuana kutafuta mrembo wa IFM kwa mwaka 2010.
Katika shindano hilo warembo watano waliibuka kuwa wawakilishi wa chuo hicho katika ngazi za juu za vyuo.
Warembo hao ni Flora Martin aliyeibuka Miss IFM mwaka 2010, Judith Osima alishika nafasi ya Pili na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Esther Emmanuel wakati nafasi ya nne ilichukuliwa na Editruda Msoka na ya tano ilinyakuliwa na Pendo Sam.
KATIKA shindano hilo mshindi wa kwanza Miss IFM Flora Martin aliibuka na zawadi ya Laptop yenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 na pesa taslimu shilingi 300,000, mshindi wa pili alizawadiwa Dressing table yenye thamani ya shilingi 500,000 na pesa tasilimu shilingi 200,000.
Mshindi wa tatu aliibuka na TV aina ya Hitachi inchi 24, na kiasi cha shilingi 150,000.
Mshindi wa Nne na watano waliondoka na mshiko wa shilingi 120,000.
Jumla ya zawadi zote zilizoandaliwa katika shindano hili ziligharimu kiasi cha shilingi milioni 3.5.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment