Saturday, October 9, 2010
Liverpool hatarini kupoteza pointi
Liverpool hatarini kupoteza pointi
Klabu ya Liverpool inakabiliwa na hatari ya kukatwa pointi tisa iwapo kampuni inayoimiliki ya Kop Holdings itafilisiwa wiki ijayo.
Kanuni za ligi zinaeleza pointi zinaweza kukatwa iwapo kampuni inayoimiliki inakabiliwa na hatari ya kufilisika kutokana na mzozo wa utawala.
Taarifa zilizopatikana zinasema wamiliki wa klabu hiyo Tom Hicks na George Gillett watakuwa na kibarua kigumu kujieleza kwamba uendeshaji wa klabu hiyo hauathiri kampuni yao.
Liverpool inaweza ikaingia katika wimbi la kutangazwa imefilisika iwapo uuzwaji wa klabu hiyo hautakuwa umekubalika itakapofika tarehe 15 mwezi huu wa Oktoba.
Iwapo Hicks na Gillett watafanikiwa kuzuia uuzwaji wa klabu hiyo kwa gharama ya paundi milioni 300 kutoka kwa kampuni ya New England Sports Ventures (NESV), wanaomiliki timu ya mchezo wa baseball ya Marekani ya Boston Red Sox , kampuni yao inaweza kutangazwa imefilisiwa na Royal Bank of Scotland kutokana na deni inayodai ya paundi milioni 280.
Mtendaji Mkuu wa bodi inayoendesha Ligi kuu ya England Richard Scudmore, mwenyekiti Sir Dave Richards na katibu Mike Foster ndio watakaoamua kama kuna haja ya kuikata pointi klabu hiyo.
Liverpool tayari ipo katika wimbi la timu tatu zilizo chini ya msimamo wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuanza vibaya msimu huu ikiwa na pointi sita tu kutokana na michezo saba iliyocheza hadi sasa.
Awali ilifikiriwa klabu hiyo ingeweza kuepuka adhabu hiyo, lakini sasa inakabiliwa na hatari iliyo wazi ya kukatwa pointi iwapo uuzaji wa klabu hiyo kwa kampuni ya NESV utacheleweshwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment