Sunday, October 3, 2010

Nyota wa R&B Matatani Kwa Kumpiga Mama Yake



Nyota wa muziki wa R&B, Mario Barret, au maarufu kama Mario amefunguliwa mashtaka kwa kumshambulia mama yake aliyekuwa akiishi naye katika nyumba yao iliyopo Baltimore, Maryland nchini Marekani.

Maafisa wa polisi waliitwa nyumbani kwao ambapo mama wa nyota huyo wa muziki, Shawntia Hardaway, aliwaambia kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 24 amemjeruhi.

Shawntia aliwaambia polisi kuwa Mario alimsukuma na kukibamiza kichwa chake ukutani na kumsababishia maumivu makali ya kichwa.

Shawntia aliongeza kuwa anahofia maisha yake kutokana na kwamba hilo ni tukio la pili mtoto wake amemshambulia ndani ya wiki moja.

Mwanasheria wa Mario, William "Hassan" Murphy III, alisema kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya kati ya mtoto mwenye mapenzi na mama yake ambaye anatumia madawa ya kulevya.

Mario alifunguliwa mashtaka na yuko nje kwa dhamana ya dola 50,000.

No comments:

Post a Comment