Saturday, October 9, 2010

Man United yadaiwa paundi milioni 80


Man United yakabiliwa na deni kubwa



Klabu ya Manchester United imearifiwa inadaiwa paundi milioni 79.6 za Uingereza hii ni kabla ya kukatwa kodi, ikiwa ni mzozo mkubwa wa kifedha kuikumba klabu, hiyo hali iliyosababisha kupungukiwa na fedha za mauzo ya wachezaji.





Deni hili ni la miezi 12 hadi mwezi wa Juni, ikilinganishwa na faida ya paundi milioni 48 kwa mwaka uliopita, ambapo mapato yaliongezeka baada ya kumuuza mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo kwa paundi milioni 80.

Madeni yote kwa ujumla ya klabu hiyo kwa mwaka uliopita yalifikia dola milioni 67. Pia klabu hiyo ililipa riba ya paundi milioni 40.

Wakati watu nao walipungua kuingia uwanjani kwa mechi, hali iliyozidisha kuporomosha mapato ya kibiashara ya klabu.

Kwa ujumla mapato halisi ya Manchester United kwa mwaka yaliongezeka kwa paundi milioni 286.4.

Malipo ya riba ya paundi milioni 40 yaliyofanywa yalikuwa sawa na malipo ya mwaka uliopita.

Faida itokanayo na uendeshaji, ambayo haijumuishi gharama za madeni yaliyotokana na huduma, pia imepanda, na kufikia paundi milioni 100.8, ikilinganishwa na paundi milioni 92 kwa mwaka uliotangulia.

Manchester United ilinunuliwa na familia ya akina Glazer ya Marekani kwa dola milioni 800 mwaka 2005.

Mashabiki wanaoipinga wanadai familia hiyo imeitumbukiza klabu hiyo katika deni kubwa, hali iliyosababisha kuwepo na maandamano.

Mashabiki wengi wanaendelea kususia kuvaa fulana za klabu hiyo za rangi nyekundu pamoja skafu na badala yake wameamua kuvaa fulana za rangi ya kijani na dhahabu, ambazo ndio rangi za asili za Newton Heath, klabu iliyoanzishwa mwaka 1878 iliyokuwa an wachezaji wasio wa kulipwa ambayo baadae iligeuka na kuwa Manchester United.

No comments:

Post a Comment