Saturday, October 9, 2010

Fifa kuwaondoa mawakala wa wachezaji



Fifa inatarajia kuondoa utaratibu wa kuwatumia mawaka kwa sababu asilimia 30 ya uhamisho wa wachezaji wa kimataifa unasimamiwa na mawakala wenye leseni.


Rais wa Fifa, Sepp Blatter


Chama cha Soka cha England kimewaambia mawakala huenda kuanzia mwezi wa Oktoba mwaka 2011 maombi mapya ya watu wanaotaka kuwa mawakala wenye leseni hayatapokelewa".

Mshauri wa soka Tor-Kristian Karlsen, ameiambia BBC: "Suala la mawakala halitakuwepo."

"Kwa hika ni vurugu tupu na huchukua muda mrefu kwa Fifa kufuatilia na kukagua na hakika ni suala lenye urasimu."

Katika suala zima la uhamisho wa wachezaji, mawakala wanawashauri wachezaji juu ya udhamini na haki zao pamoja na mambo mengine na kwa kawaida hulipwa kiasi fulani fedha kutokana na mapato ya mkataba wa mchezaji, kawaida huwa kati ya asilimia 5 hadi 10.

Kazi ya mawakala zaidi wanashughulika na uhamisho wa wachezaji na wanaweza kufanya kazi muhimu sana ya kusimamia mikataba ifanikiwe.

Utaratibu wa sasa wa Fifa unaohusu mawakala wa wachezaji ulianza kutekelezwa tarehe 1 Januari 2008, lakini mwaka uliopita, kitengo kazi cha Fifa kilikuwa kikikutana mara kwa mara kupitia upya namna utaratibu huo unavyofanya kazi.

Kikundi kazi hicho kitatoa taarifa yake mwishoni mwa mwaka 2010 na utaratibu mpya unatarajiwa kuanza baada ya mwezi wa Mei mwaka 2011, huku Fifa ikisisitiza kuliko kuupitia upya utaratibu wa mawakala, inaona ni vyema kuwa na watu binafsi watakaowakilisha wachezaji ama klabu".

Lakini kutokana na asilimia 70 ya uhamisho wa wachezaji wa kimataifa ukisimamiwa na mawakala wasio na leseni, Fifa imeridhika utaratibu wa sasa sio mzuri

No comments:

Post a Comment