Friday, August 6, 2010

Msaada kwa vilabu vidogo England



Uongozi wa ligi kuu ya mpira wa miguu wa England utatoa kitita cha pauni milioni 375 kwa vilabu 72 vya daraja za chini kwa kipindi cha misimu mitatu ijayo.

Mpango huu umetangazwa Jumatano baada ya vilabu vinavyoshiriki kukubaliana juu ya sheria mpya kuhusu fedha.

Ikiwa ni sehemu ya malipo ya kila mwaka ya pauni milioni 124 , idadi kubwa ya vilabu vilivyo katika daraja la chini vitapokea pauni milioni 200.

Lakini kwa vilabu vilivyoshuka kutoka ligi kuu ya Premiership, vitapokea pauni milioni 48 kwa kipindi cha misimu minne badala ya pauni milioni 16 kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Vilabu vya daraja la kwanza vitapokea pauni 335,000 kwa kila mwaka, huku vilabu vya daraja la pili vitapokea pauni 225,000.

No comments:

Post a Comment