Thursday, August 12, 2010

O'Neill ajiuzulu umeneja Aston Villa .

Kevin MacDonald ameteuliwa kuwa kaimu meneja ingawa hakuna sababu yoyote ilitolewa kwanini O'Neill kaamua kuondoka baada ya kushikilia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka minne.

MacDonald ataitayarisha klabu hiyo kwa mechi yao ya kwanza ya msimu huu wa ligi kuu ya soka ya England dhidi ya West Ham siku ya Jumamosi.

O'Neill, ambae aliteuliwa mwaka 2006, alisema : "Nimefurahia mno kipindi nilichotumikia Aston Villa. Ni wazi kabisa kwamba itakuwa machungu mno kuiacha klabu nzuri kama hii."

O'Neill mwenye umri wa miaka 58 ambae kwa msimu wa tatu mfululizo aliiongoza klabu ya Villa na kushikilia nafasi ya sita katika ligi kuu ya soka ya England aliwasifu wachezaji wa Villa na wasaidizi wake kwa mchango wao kwa klabu na kwake yeye binafsi wakati wa kipindi chake akiwa meneja.

O'Neill ameleta mabadiliko makubwa katika klabu cha Aston Villa tangu ashike nafasi ya David O'Leary mwaka 2006, na kufikia kilele kwa kufaulu kucheza fainali ya kombe Carling msimu uliopita ikiwa mara ya kwanza kucheza fainali ya Wembley katika kipindi cha miaka 10.

Lakini kumekuweko tetesi nyingi ya hali ya mvutano kati yake na mmiliki wa Villa Randy Lerner, kuhusu kuuzwa kwa mchezaji kiungo wa klabu hiyo James Milner kwa Manchester City, na kama angeweza kutumia mauzo ya mchezaji huyo kununua wachezaji wapya.

Aliyekua nahodha wa klabu hiyo Gareth Barry naye pia alihamia Manchester City msimu uliopita

No comments:

Post a Comment