Tuesday, July 20, 2010

Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?


Msanii mkongwe hapa nchini Joseph Mbilinyi aka Mr 11 Sugu, ameliteka jiji la Dar kutokana na albamu yake ya Anti Virus ambayo ndani yake amewapaka live watangazaji na viongozi wa redio ya Clouds FM.

KWa mujibu wa Mr II watangazaji hao wanadaiwa kutumia redio hiyo kwa kuwatongoza wanawake wanaokwenda pale kuomba kazi pia kuzibania kazi za wasanii ambao hawapo katika listi yao.

Mr II pia amewachana live kundi la THT Kituo cha kukuza vipaji Tanzania Kuwa kituo hicho kinatumika kinyume na ilivyotarajiwa.

Albamu hiyo ya Sugu ina nyimbo zaidi ya 14 lakini hapa nchini haziwezi kupigwa katika vituo vya redio kutokana na kujaa matusi ya hadharani, hivyo albamu hiyo imekuwa ikiuzwa chini kwa chini na watanzania wengi wamekuwa wakiishambulia kwa kuinunua hasa wale wapenda mapinduzi katika fani hiyo ya muziki wa kisasa kwani vijana wengi wamekuwa wakibaniwa kazi zao kutokana na kutofahamika au kutokana na kutokuwa na uhusiano muzuri na watu wa redio na Tv.

Majuzi Sugu alikamtwa na polisi na kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano, lakini baadaye aliachiwa kwa dhamana.

MR II amewaweka njia panda watangazaji wa Clouds hasa kwa kuwataja live baadhi ya watangazaji kuwa wanasambaza Ukimwi kwa makusudi huku wakijua kuwa wao ni waathirika wa ugonjwa huo.

Pia aliwataja baadhi watangazaji kuwa ni wasenge jambo ambalo limewafanya watu wengi wajiulize imekuwaje hadi Mr II ameamua kutunga nyimbo hiyo na kuisambaza kwa watanzania?.

"Hapa kuna jambo ambalo kiuhakika litakuja kujulikana siku zijazo kwanini nyimbo hizo zitungiwe tu watangazaji wa Clouds, huku vyombo lukuki vikiwa vipo na havikutajwa hata kimoja?", alisema mmoja wa wadau wa muziki wa Bongo Fleva aliyehojiwa na Nifahamishe kuhusiana na albamu hiyo ya Sugu.

Angalia video ya wimbo huo chini.

No comments:

Post a Comment