Tuesday, July 27, 2010

Raul astaafu Real Madrid

Raul
Aliyekuwa mshambuliaji mashuhuri wa Hispania Raul Gonzalez ametangaza kuiacha klabu ya Real Madrid baada ya kuichezea kwa miaka 18 akidai kwamba huenda akahamia klabu ya ligi ya Primia ya England.
Raul mwenye umri wa miaka 33-alitazamiwa kujiunga na klabu ya Ujerumani ya Schalke kwa mkataba wa miaka miwli lakini alikanusha kuwepo kwa mkataba wowote.

Raul amefunga mabao 323 katika mechi 741 alizoichezea Real Madrid na mabao 44 katika mechi 102 alizozichezea Hispania.
Mbali na klabu ya Bundesliga ya Schalke kumekuweko tetesi kwamba klabu za England
kama Tottenham, Newcastle, Liverpool
na Manchester United nazo pia zinamwangaza Raul.

Mano Menezes ndiye kocha mpya wa Brazil

Kocha Mano Menezes wa timu ya klabu ya nyumbani, Corinthians, sasa ndiye kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Brazil.

Shirikisho la soka nchini Brazil, CBF, limethibitisha kwamba Menezes ameikubali kazi hiyo.

Shirikisho hilo la CBC lilimtaka Menezes, mwenye umri wa miaka 48, kuifanya kazi hiyo, baada ya mtu waliyemchagua kwanza, Muricy Ramalho, kushindwa kuikubali.

Klabu ya Fluminense ilimtaka Ramalho kuzingatia mkataba wake hadi utakapokwisha, na kuendelea hadi mwaka 2012.

Katika miaka ya hivi karibuni, Menezes ameweza kuiongoza klabu ya Corinthians, na kabla ya hapo Gremio, kutoka katika daraja ya kwanza, hadi ligi kuu.

Brazil, ambayo itakuwa ni mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, ilikuwa ikimtafuta kocha mpya, baada ya kumfuta kazi Dunga.

Hii ni kwa kuwa Brazil iliondolewa katika robo fainali, katika mashindano yaliyopita ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, mapema mwezi huu.

Menezes mwenyewe amesema; "nimeikubali kikamilifu kazi hiyo na kwa fahari kubwa, kuifundisha timu ya taifa".

Uso wa kupachikwa waonekana


Oscar na mmoja wa madaktari wake


Mhispania mmoja aliyepachikwa viungo vya uso mzima wa mtu mwengine uliofanyika kwa mara ya kwanza duniani ameonyesha uso wake ulivyo kwa sasa hadharani mbele ya televisheni.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 31 ameishukuru familia iliyomfadhili kwa kutoa viungo hivyo na wataalamu waliompa uso mpya mwezi Machi katika hospitali ya chuo cha Vall d'Hebron, Barcelona.

Kupigwa risasi kwa bahati mbaya kwa mtu huyo kulimaanisha kuwa ngozi yake ya uso na misuli-ikiwemo ya poa na midomo- kulitakiwa kubadilishwa upya.

Madaktari wamesema Mhispania huyo anaweza kutarajia hisia zake za uso kurejea kwa asilimia 90.

Baada ya kupata ajali miaka mitano iliyopita mtu huyo alikosa uwezo wa kupumua, kumeza au hata kuzungumza vizuri.

Sasa mtu huyo, anayetambulika tu kama Oscar, bado anahangaika kuzungumza kwa umakini na atahitaji miezi kadhaa ya kufanyiwa matibabu ya mwili.

Alisema katika mkutano na waandishi wa habari: " Marafiki zangu, nataka kuwashukuru wasimamizi wa hospitali, wote walionipa matibabu, familia iliyonifadhili na zaidi ya wote familia yangu inayonisaidia siku hizi."

Iliamuliwa uso wa Oscar ubadilishwe upya baada ya upasuaji huo kufanyika mara tisa bila mafanikio.

Kundi la wataalamu 30 lilifanya upasuaji huo uliodumu kwa saa 24 tarehe 20 Machi huko Barcelona.

Ukiongozwa na Dr JP Barret, timu hiyo imerekebisha misuli, pua, midomo, taya, paa la kinywa, meno yote, kitefute (cheek bones), na utaya kwa njia ya upasuaji.

Ni upasuaji wa mwanzo wa uso mzima kufanyika duniani, kwani nyengine 10 zilizofanyika hapo awali zilikuwa sehemu tu ya uso.

Mafanikio ya mwanzo ya upachikaji wa viungo vya uso kwa mtu mwengine ulifanyika nchini Ufaransa mwaka 2005 kwa Isabelle Dinoire, mwanamke wa umri wa miaka 38 ambaye aliumizwa vibaya na mbwa wake.

Saturday, July 24, 2010

MBAYA WANGU YUKO WAPI?


Kama ipo wiki ambayo nilitamani sana ifikie ukingoni,hii bila shaka ni mojawapo.Kwa kiasi fulani nilikuwa nimeshachoka na “watangaza nia”.Naona kila mtu anaitumia ipasavyo haki yake ya msingi.Watetezi wanasema huo ndio ukuaji wa demokrasia.


Wasiwasi wangu ni kwamba kwa namna fulani,imeshageuka kuwa fasheni.Si unajua tunavyopenda kuigana?Mmoja akianza kitu basi wengine ni lazima wafuate.Unataka kuniambia umesahau biashara ya salon ilipoanza? Au daladala za watu binafsi ziliporuhusiwa?


Kwa “waliotangaza nia” na kuchukua fomu, naomba uwasikilize kwa makini.Sentensi na misemo inakuwa ni ile ile.Ahadi zinakuwa zinafanana.Huyu akiahidi kwamba ataanzisha kituo cha televisheni mahali ambapo hata umeme haujafika,mwingine bila hata kufikiria naye anasema hivyo hivyo.Mwananchi wa kawaida,kichwa kinapata kizunguzungu.Amwamini nani?Mbona wote wanaongea sawa na ahadi zao zinafanana? Labda nikamsikilize kasisi kanisani au sheikh msikitini? Mmh huko nako kuna mengi.Kama jiwe la msingi liliwekwa na fulani,kuna jipya?


Kwa hiyo nikawa natamani wikiendi iwadie kwani sijasikia sana kuhusu wanaotangaza nia katika siku za wikiendi.At least sio hadharani.Labda kule kwenye moja moto,moja baridi.Kichwa kikianza kuwa kizito,lugha inabadilika na sera za kweli zinaanza kutolewa.Ngoja wanichague,I can’t wait kuwa na “shangingi” langu na dereva.Mimi na safari,safari na mimi.Pembeni toto ya kona.Mheshimiwa Mbunge(MP).


Enewei,maisha yanasonga.Burudani ni jadi yetu hapa.Wimbo wa leo unaitwa Namsaka Mbaya Wangu
kutoka kwao Dar-es-salaam Jazz Band chini ya Jabali la Muziki,Hayati Marijani Rajabu.


Dar-es-salaam Jazz Band ni mojawapo ya bendi za kwanza kwanza kubwa nchini Tanzania.Ni bendi ambayo wanamuziki wengi sana wakongwe walipitia.Kwa mfano kina Ahmed Kipande, Patrick Balisidya, Juma Mrisho, Dancan Njilima, Moshi William (Tx), Juma Akida, Emmanuel Joseph, Hamis Nguru na wengine wengi.Iliundwa kufuatia mmeguko kutoka bendi iliyokuwa inajulikana kama African Association Jazz Band iliyokuwa na makao yake makuu,Kariakoo katika miaka ya 30s. Katika miaka ya 30s mpaka 40s bendi kubwa zilibakia kuwa African Association Jazz Band na Dar-es-salaam Jazz Band.


Baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Dunia ya Pili,huku veterans wakirejea huku wakiwa na santuri mbalimbali kutoka ughaibuni,picha ya starehe za mjini nazo zikaanza kubadilika kidogo.Meneja wa Dar Jazz Band wakati huo alikuwa jamaa aliyeitwa Athumani Muba(Mzee Muba) ambaye alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa bendi hiyo pamoja na kina Hamisi Machapati.In fact nyumba yake pale mitaa ya Kariakoo-Gerezani ndio ilikuwa “clubhouse”.


Baadaye katika miaka ya 60s bendi hiyo ilikuwa chini ya uongozi wake Michael Enoch,mpiga gitaa la solo maarufu ambaye inasemekana ndiye Mwalimu wa wanamuziki wengi sana nchini Tanzania.Baadaye Enoch alikuja kuwa mpiga saxophone mzuri na ambaye saxophone yake inasikika katika nyimbo nyingi zilizotamba za Mlimani Park Orchestra(Sikinde) alikohamia baadaye.


Lakini kwa wengine wengi,Dar Jazz Band inayokumbukwa ni iliyokuwa chini ya Jabali la Muziki,Marijani Rajab(RIP)

Rashid Matumla au ukipenda “Snake Boy”, juzi ilikuwa ndio mwisho wake


Kila jambo lina mwisho wake. Kwa Bondia mkongwe na mahiri nchini Tanzania,Rashid Matumla au ukipenda “Snake Boy”, juzi ilikuwa ndio mwisho wake katika mchezo wa ndondi akiwa kama mchezaji.


Baada ya pambano lake na Bondia mwingine anayekuja juu katika mchezo huo,Mada Maugo,lililofanyikia katika Ukumbi wa PTA uliopo kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Matumla alitangaza kustaafu rasmi au kutundika “gloves” kama wenyewe wanavyosema.Katika pambano hilo,Matumla alipoteza kwa jumla ya pointi 98-95.Pambano hilo ambalo halikuwa la kuwania ubingwa wowote,lilikuwa la raundi kumi.


Matumla ambaye aliyewahi kufanya makubwa katika medani ya ngumi za kulipwa, alifikia hatua hiyo baada ya miaka kadhaa kushauriwa na wadau kadhaa akiwamo baba yake mzazi kuachana na mchezo huo kutokana na umri kumtupa mkono, bila mafanikio.


Rashid Matumla alizaliwa tarehe 16/5/1968 mkoani Tanga. Mpaka anastaafu na tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa,ameshinda mapambano 40(kati ya hayo 30 kwa Knock Out) na ameshindwa katika mapambano 14(manne kati ya hayo alipigwa kwa KnockOut) na ametoka draw katika mapambano 2. Kwa ujumla amepambana katika raundi 373. Mpaka anastaafu katika ulimwengu wa ndondi za kulipwa katika uzito wa kati(Middle Weight),Matumla anashikilia nafasi ya 299 kati ya wanandondi 1107 wanaotambulika na walio active katika uzito huo.Kwa nchini Tanzania,amestaafu akiwa katika nafasi ya 5 miongoni mwa mabondia 29 wanaotambulika na ambao bado wapo active.Walio mbele yake ni Karama Nyilawila,Thomas Mashali,Mada Maugo, na Francis Cheka ambaye ndiye nambari 1 kwa hivi sasa nchini Tanzania.


Baada ya kustaafu Matumla amesema ushiriki wake katika mchezo huo namba mbili kwa kuwa na wapenzi wengi duniani nyuma ya soka,utakuwa katika nafasi ya ukocha.Amesema hivi sasa atajikita katika kuibua vipaji vya ndondi miongoni mwa vijana.


Tunamtakia Rashid Matumla au “Snake Boy” maisha mema katika kustaafu.

siku ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela-Madiba.

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela-Madiba.Anatimiza miaka 92.On behalf of the entire team of BC,it’s readers,contributors and all well wishers, we wish you Madiba a Happy Birthday.May you live many many more years!
11th February,1990.A walk out of prison after 27 years!

Mimi ni Kidum .Nataka kutoa maelezo

Mimi ni Kidum .Nataka kutoa maelezo kikamilifu kuhusiyana na iyi muzozo wa uyu wimbo wangu na Lady Jaydee .Hakuna shida yeyote yipo kati yangu na Hermy B ambayo ni producer wa round ya kwanza ya recording ya uyu wimbo .

Kama vile munajuwa mimi naishi nairobi na hapa ndipo nafanya shuhuli za muziki wangu kwa muda mrefu .Sasa kama kwa mfano nime rekodi Dar es salaam alafu nisikiye kuna hitirafu kidogo kwa wimbo ni ngumu niwe nachukuwa ndege kila mara nikikuja Dar es salaam ingawa napapenda sana wakati hapa nairobi piya kuna studios .

Kwa mfano version ya kwanza Key ile tuliimbiya mimi na jaydee ni yenye ambao ilikuwa chini sana kuweza kuwa rahisi kwa mwana dada lakini tulipo rudiya sasa mwana Dada sauti yake ikatoka kama ya malaika .Hapakuwa ubaya wakurudiya ku rekodi tena uyu wimbo sababu mimi mwenyewe niko msanii na kuna kile kitu mimi natafuta kwa hali ya ubora zaidi kama sikipati bila shaka ata ku rekodi mara ya tatu siwezi kusita kufanya . Wimbo ni wangu mimi na lady jaydee sisi wenyewe tukielewana na tu amuwe kuwurudiya sioni kama kuna ubaya .
Hata Hermy B mwenyewe na amini munamusemeya uwongo ya kwamba anamatatizo kuhusiyana uyu wimbo sababu mimi mwenyewe naelewa vema kwenye radio stations nyingi wanacheza version yake ya Audio . bado ni uyo wimbo tu iwe video ama audio .Na pia bado ni Kidum na Lady Jaydee iwe ni video ama ni Audio

JAMHURI JAZZ BAND, ONDOA WASIWASI


Sijui wewe mwenzangu,ila mimi nahisi siku zinakwenda kwa kasi ya ajabu.Wiki inavyokatika huwa nashindwa kujua hata imeishaje! Nikizingatia kwamba tayari tupo katika ngwe ya pili ya mwaka 2010,napata wasiwasi kidogo.Je ntatimiza malengo yangu niliyojiwekea siku ile ya mwaka mpya wakati ving’ora vikilia kutoka bandarini,taa zikiwaka na kuzimika?

Pamoja na kupatwa na wasiwasi ninapoangalia mzunguko wa saa,huwa napata faraja kujua kwamba wiki ndio inakatika na kwa maana hiyo,weekend imewadia.Ni muda wa kupumzisha akili kidogo.Ni muda wa kuburudika na “Zilipendwa” kama ilivyo jadi yetu hapa BC. Najua pengine bado unawajibika wakati wa weekend.Sawa.Lakini kuna pumziko fulani.Barabarani magari yanakuwa yamepungua.Mitaani kunakuwa kweupe kidogo.

Kwa upande mwingine,fainali za Kombe la Dunia la FIFA ndio zishamalizika.Pweza Paulo kajipatia umaarufu wa kutosha.How could he be right all the time? Naambiwa sio Paulo Pweza peke yake aliyekuwa sahihi katika utabiri.Nasikia hata Spika wa Bunge letu,Mheshimiwa Sitta alitabiri kwamba Spain “itafanya vizuri sana”. Lakini kali ni kutoka kwa Nabii Joshua(kama hujawahi kumsikia nisamehe).Yeye alitabiri vyema kabisa mechi ya ufunguzi katika ya South Africa na Mexico. Alisema Mungu kamwambia South Africa watafunga goli kwanza ila wasipolilinda litarudishwa!.Upo hapo? Mambo ya common sense hayo.

Enewei,fainali zimeisha vyema.Afrika Kusini wametutoa kimasomaso maana jamaa wa magharibi walikuwa wamechachamaa kweli wakisema Afrika hakuna nchi inayoweza kuandaa mashindano makubwa kama yale. Kumbe hawakujua kwamba waafrika,pamoja na mambo yetu yote,tunasikilizana.Wale “chinjachinja” wakaambiwa tulizeni mzuka wakati wa fainali na kweli jamaa wakatulia kimyaa.Ngoma ipo kwa Brazil sasa.Jamaa wanaanda fainali za mwaka 2014.Kule napo nasikia fujo kama kawaida.Kuna Favela.

Turudi kwenye burudani sasa.Leo tunao Jamhuri Jazz Band.Wimbo unaitwa Wasiwasi Ondoa. Jamhuri Jazz Band ilianzishwa katika miaka ya 50s kule mkoani Tanga.Wakati huo kulikuwa hakuna Tanzania bali Tanganyika.Mwanzoni bendi hiyo iliitwa Young Nyamwezi Band.Mabadiliko yalifuata baada ya kupata ufadhili wa bwana mmoja aliyeitwa Joseph Bagabuje.Baadaye Bagabuje alikuja kuwa mtanganyika wa kwanza kuwa Meneja wa Amani Tea Estate.

Miongoni mwa wanamuziki ambao baadaye walijiunga na bendi hiyo na kuisaidia kukua zaidi ni pamoja na wana-ndugu Wilson Kinyonga na George Kinyonga. Walijiunga na Jamhuri Jazz Band mwaka 1966 kabla hawajimega mwaka 1970 na kwenda kuunda Arusha Jazz Band na baadaye Simba Wanyika.

Lundega: Miss Tanzania mwaka huu balaa


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency ambayo ndiyo waandaaji wa mashindano hayo, Hashimu Lundenga 'Uncle Hashimu'.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Lundenga alisema kuwa tofauti na miaka yote, mwaka huu kila sehemu wamejitahidi kutoa warembo wenye sifa za urembo hivyo kuongeza ushindani zaidi.

"Tulivyoona tu katika mikoa ambayo imeshapata wawakilishi wao, kuna warembo wengi wenye vigezo haswa vya kutwaa taji hili, kwa hiyo hatujui ni mkoa upi hasa mwaka huu utatwaa taji hilo," alisema Lundenga.

Mwaka jana mkoa wa Mwanza ndiyo ulioibuka kidedea baada ya mlimbwende wake Mariamu Gerald kuibuka kidedea na kutwaa taji hilo.

Fella Ageukia Qaswida


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Fella alisema kuwa ameamua kukisaidia chuo hicho ambacho kiko Mbagala Kizuiani kutoa albamu ikiwa ni harakati ya kutangaza habari za mungu kupitia Qaswida.

"Hiki ni chuo ambacho mimi nilisoma, kwa hiyo nimeona ni vyema nikawasaidia kutoa albamu hii ili waweze kufikisha ujumbe wao kwa jamii kupitia Qaswida," alisema Fella.

Fella alisema kuwa albamu hiyo ambayo tayari imeshaingia sokoni ina nyimbo nne ambazo ni Mazingira uliobeba jina la albamu, Ukimwi na Ndoa.

Alisema kuwa anaamini Qaswida kama zitapewa nafasi zinaweza kufanya vyema katika ulimwengu wa muziki na kusaidia vilivyo kuiweka jamii katika mstari ulionyyoka.

"Qaswida mara nyingi nyimbo zake ni zile ambazo haziipotoshi jamii, na ni muziki ambao wahusika wake wanatakiwa kuweka mbele huduma zaidi za kijamii ukilinganisha na gospo ambao umegeuka kuwa muziki wa kibiashara zaidi," alisema Fella.

Friday, July 23, 2010

O'Neil yuko tayari kumwuuza Milner


Meneja wa Club ya Aston Villa Martin O'Neill anasema yuko tayari kumuuza mcheza kiungo wake James Milner baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia yake ya kuihama club hiyo.

Tayari Man City ilijaribu kuleta pauni milioni 20 zilizokataliwa na Aston Villa.

Kocha wa Aston Villa amesema mchezaji huyo aliyepewa muda zaidi wa kupumzika kufuatia kushiriki michuano ya Kombe la Dunia atarejea hivi karibuni na labda Man City watarudi na kitita kikubwa zaidi.

Wakati huo huo kampuni ijulikanayo kama EA Sports, maarufu kwa mpangop wake wa 'Fifa Soccer', imeafikiana na ligi ya Premiership kama mshirika wake katika teknolojia ya michezo.

Hata hivyo takwimu kuhusu gharama na fedha zinazohusika hazikutajwa, ingawa EA Sports itapewa haki zaidi katika mipango ya ligi kuu ya England.

Miongoni mwa kazi zinazotarajiwa na kampuni hiyo ni matangazo ya kampuni hiyo kwa mechi zote zitakazotangzwa moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kupitia vituo vya kibiashara kama Sky Sports, ESPN na vingine vya kimataifa.

Pamoja na hayo kampuni hiyo itatoa takwimu za timu bora ya wiki kwenye wavuti yake ya Ligi ya Premier ya England.

Jol kuifunza Fulham


Martin Jol anatazamiwa kutajwa kuwa meneja mpya wa Fulham.

Kwa mujibu wa idara ya michezo ya BBC, kocha huyo wa Ajax amekuwa na mazungumzo ya awali na klabu hiyo ya London, na kuwa atazungumza na maafisa wa Fulham baadaye wiki hii kuzungumzia mkataba wake.


Martin Jol kurejea tena London

Jol, mwenye umri wa miaka 54 aliwahi kuifundisha klabu nyingine ya London ya Tottenham kati ya mwaka 2004 na 2007. Anatazamiwa kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliyejiunga na Liverpool tarehe mosi mwezi Julai.

Kocha wa Ivory Coast, Sven Goran Ericksson alikuwa pia akitajwa kuchukua nafasi hiyo ya Fulham. Hakutakuwa na taarifa rasmi kuhusu kuteuliwa kwa Jol, kabla ya Fulham kwenda Sweden kwa ajili ya michezo ya kabla ya msimu kuanza, lakini Jol anatarajiwa kuungana na kikosi hicho baadaye.

Kocha wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley na kocha wa Uswisi Ottmar Hitzfield pia walikuwa wakitajwa, lakini Hitzfield alijitoa, huku taarifa ya chama cha soka cha Marekani ikisema itaongeza mkataba wa kocha wake wa taifa.

Jol aliyefukuzwa kazi na Tottenham mwezi Oktoba mwaka 2007, bado anamiliki nyumba nchini England na taarifa zinasema raia huyo wa Uholanzi atapewa mkataba wa kuendelea. Ingawa Fulham ilicheza fainali ya ligi ya Europa mwezi may mwaka huu, Ajax itakuwa ikicheza ligi ya mabingwa wa Ulaya mwezi Septemba, iwapo itaweza kufuzu.

Mwisho Arudi kwa Kishindo Big Brother


Nyota ya Mwisho ilianza kung'ara wakati washiriki wa kinyang'anyiro hicho walipowasili katika jumba la Big Brother na kuwafanya watu wengi waliokuwa ndani na nje ya jumba hili kumshangilia kwa nguvu.

Akiwa amevalia nadhifu, koti lililomkaa vyema, akiwa ametupia lubega la kimasai shingoni huku akiwa amevaa hereni katika masikio yake yote mawili, Mwisho alionekana kuwa mwenye furaha na alipoulizwa anajisikiaje namna alivyopokelewa, Mwisho alisema kuwa anashindwa kuelezea.

Mwisho pia alisema kuwa kwa hivi sasa maisha yake anayaendesha kijiji kwao Morogoro, na anafurahia maisha ya huko kwa sababu mbali ya kulima, lakini pia anapata fursa ya kufurahia maisha na wanakijiji.

Watanzania waliohudhuria katika hafla maalumu ya uzinduzi wa shindano hilo, uliofanyika katika hoteli ya Holiday In jijini Dar es Salaam, walifurahishwa na uwakilishi wa Mwisho na kusema kuwa wana matumaini makubwa kuwa atafanya vyema.

"Mwisho ni mshiriki mwenye mvuto kuliko washiriki wote wa Tanzania na tunamatumaini atafanya vyema kama alivyofanya awali," alisema msanii mahiri wa filamu nchini, Jacob Steven 'JB'.

"Siyo siri jamaa anapendwa. Anakubalika kwa kweli. Nyota yake bado iko juu. Mimi nakuambia Mwisho atawafanya watanzania wayafuatilie tena mashindano hayo kwa ukaribu mno." alisema Miss Tanzania Miriam Gerald ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

Washiriki walioingia katika jumba hilo ni Paloma Manda kutoka Zambia, Jeniffer Mussanhane (Msumbiji), Dj Code Sangala (Malawi), Samwel Kwame Bampoe 'Sammy B' (Ghana), Maureen Namatovu (Uganda), Jacob Yehdego (Ethiopia), Munyaradzi Hidzonga (Zimbabwe).

Wengine ni Sheila Kwamboka (Kenya), Meryl Shikwambane (Namibia), Uti Nakumbe (Zimbabwe), Lerato Sengadi (Afrika Kusini), Kaone Ranantshonyana (Botswana) na Hannington Kuteesa(US).

Tuesday, July 20, 2010

Warwanda 'wana uhuru wa kuchagua"

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameahidi uchaguzi wa mwezi ujao utakuwa huru, akipinga ukosoaji wa hivi karibuni uliotolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Akizindua kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Agosti 9, " Wapiga kura wa Rwanda wana uhuru wa kuchagua."

Wakosoaji kadhaa wameuliwa au kushambuliwa hivi karibuni, afisa mmoja mwandamizi alikuwa akizikwa huku Bw Kagame akiwa anazungumza.
Serikali imekana kuhusika na mauaji yeyote.

Mwandishi wa BBC Geoffrey Mutagoma mjini Kigali amesema maelfu ya wafuasi wa Bw Kagame- wengi wakiwa wamevaa rangi za chama ikiwa ni nyekund, nyeupe na bluu- wamejaza uwanja wa taifa wa Amahoro na wengi wameshindwa kuingia.

Vyama vingine vitatu vimezindua kampeni zao lakini vyote vinaonekana kuwa karibu na Rais- viwili vimekuwa serikalini tangu mwaka 1994.

Vyama vingine vingi vya kisiasa vimezuiwa kushiriki katika uchaguzi.

' Si mjinga'
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kampeni hizo, Bw Kagame alisema anahisi chama chake kitarudi madarakani: " Nina imani kuwa raia wa Rwanda watachagua kushirikiana na RPF."

Saa chache kabla ya kampeni kuanza, makamu wa Rais wa chama cha Democratic Green, Andre Kagwa Rwisereka alizikwa.

Mwili wake ambao karibu wote ulikuwa umekatwa ulikutwa Butare kusini mwa Rwanda wiki iliyopita baada ya kuripotiwa kutojulikana alipo.

Chama chake hakiwezi kushiriki kwenye uchaguzi, na kinadai serikali imekataa kukisajili.

Kumekuwa na matukio mengine yaliyozua wasiwasi katika miezi ya hivi karibuni, ikiwemo kifo cha mwandishi maarufu wa habari, jaribio la kumwuua aliyekuwa mkuu wa majeshi, na wengi kukamatwa huku kukiwa na ripoti za kugawanyika katika jeshi la Rwanda.

Serikali imekana kuwavuruga upinzani.

Waziri wa mambo ya nje Louise Mushikiwabo ameliambia shirika la habari la AP, " Najua wengi hawatotuona kama ni serikali ya kuigwa, lakini si wajinga, na hatutajaribu kuua watu watatu kwa mpigo kabla ya uchaguzi- uchaguzi ambao tunaamini kuwa Rais Paul Kagame atashinda."

Lakini mwandishi wetu alisema si kila mmoja anaamini kauli hiyo.

Raia wa kigeni wajeruhiwa Afrika Kusini


Takriban raia wa kigeni wanne wamejeruhiwa katika kitongoji cha Kya Sands nchini Afrika Kusini, mjini Johannesburg katika mashambulio yanayowalenga raia wa nje ya nchi hiyo.

Msemaji wa polisi amesema walikuwa pia wakichunguza taarifa za uporaji.

Mwandishi mmoja wa habari wa Johannesburg alisema maafisa wa polisi walitumia risasi za mpira, gari la kujihami na helikopta ili kuzuia mapigano hayo.

Tangu Kombe la Dunia kumalizika, kumekuwa na wasiwasi wa kuibuka upya mashambulio dhidi ya raia wa kigeni yaliyotokea mwaka 2008.

Takriban watu 62 waliuawa katika vurugu hizo wakati raia wa Afrika Kusini walipowalaumu wafanyakazi wa kigeni kwa kuchukua kazi na makazi yao.

Idara inayotoa huduma za dharura mjini Johannesburg imesema iliwapeleka 'takriban watu watano' hospitalini baada ya kupigiwa simu juu ya ghasia hizo.

Msemaji wa polisi amesema watu wanne walishambuliwa.

Serikali imekuwa ikijaribu kuzima wasiwasi wa kutokea mashambulio dhidi ya raia wa kigeni tangu Kombe la Dunia kumalizika mapema mwezi huu- iliyoandaliwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Maelfu ya wafanyakazi wa muda waliokuwa wamepata ajira wakati wa mashindano hayo wameachishwa kazi tangu imalizike Julai 11.

Mwishoni mwa juma, chama tawala cha African National Congress (ANC) kiliandaa maandamano kupinga mashambulio hayo mjini Johannesburg.

Lakini jitihada zao hazijawazuia watu kuhama na siku ya Jumatatu, serikali ya Zimbabwe imesema itaandaa hifadhi za muda katika maeneo mbalimbali mpakani kwa Wazimbabwe wanaoondoka Afrika Kusini kufuatia vitisho vya kushambuliwa kwa raia wa kigeni.

Madzudzo Pawadyira, mkuu wa idara ya usalama wa raia ameiambia shirika la habari la AFP , " Tumeweka mahema makubwa matatu huko Beitbridge, blanketi 10,000, makasha 20 ya sabuni na ndoo 1,000."

Takriban Wazimbabwe milioni tatu wanaishi Afrika Kusini, baada ya kukimbia kufuatia kudhoofu kwa hali ya uchumi na ghasia za kisiasa nyumbani.

Afghanistan yataka kujidhibiti kiusalama


Kiongozi wa Afghanistan Hamid Karzai ametoa wito upya kwa nchi yake kudhibiti usalama wake ifikapo mwaka 2014 katika mkutano mkubwa wa kimataifa mjini Kabul.

Alikiri kuwa Afghanistan bado haijafanikiwa katika utawala bora.

Alikuwa akizungumza na wawakilishi kutoka mataifa 70 kwenye mkutano mkuu wa misaada uliowahi kutokea katika kipindi cha miongo mitatu.
Marekani na washirika wake walitoa wito wakitaka Bw Karzai kutoa ahadi kuimarisha utawala bora.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Rais wa Afghanistan aliahidi wazi kupambana na rushwa huku akiimarisha amani na maridhiano.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuondoa majeshi ya nchi hiyo ifikapo 2014 ni lengo linalowezekana.

Alisema mjini Washington kabla ya kufanya mazungumzo na Rais Barack Obama, " Tunatoa mafunzo kwa jeshi la Afghanistan kila mwezi na lengo hilo linaweza kutekelezwa."

Wachambuzi wanasema kwa kuwa wapiganaji bado wanadhibiti eneo kubwa Afghanistan, Bw Karzai ana nia thabit juu ya malengo ya usalama wa nchi yake.

Lakini Bw Ban, alisema haijawahi kutokea kukawa na mwelekeo mzito wa maisha ya usoni ya Afghanistan.

Mwanamuziki Aliyejiua Kutofanyiwa Sala za Maombi Kanisani


Mwanamuziki nyota wa Romania ambaye alijiua mwenyewe kwa kunywa sumu ya wadudu hatasaliwa misa kamili ya mazishi kutokana na kanisa la orthodox la nchini humo kusema kuwa amefanya dhambi kubwa kwa kujiua.
Kanisa la orthodox la nchini Romania limegoma kumfanyia misa kamili ya mazishi nyota wa muziki wa nchini humo kwakuwa alijiua mwenyewe.

Nyota wa muziki mwanamke Madalina Manole alijiua mwenyewe kwa kunywa sumu kali ya wadudu siku ya jumatano ambayo pia ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na kutimiza umri wa miaka 43.

Mwili wa Manole uligunduliwa na mume wake wakati huo Manole alikuwa tayari ameishaiaga dunia baada ya kunywa sumu.

Kanisa la orthodox limesema kuwa mchungaji mmoja atafanya misa fupi sana kwaajili ya Madalina Manole ambayo itafanyika katika maeneo ya nje ya kanisa.

Kanisa hilo linaamini kuwa mtu kujiua ni dhambi kubwa sana.

Manole atazikwa siku ya ijumaa katika mji wake wa Ploiesti kaskazini mwa jiji la Bucharest.

Manole alikuwa maarufu sana kwa miziki ya country akitamba zaidi kwa mashairi yake ya mapenzi. Kifo chake kimewashtua watu wengi sana nchini Romania

Mwanamama avaa gauni la spinachi Kenya


Mwanaharakati aliyevaa gauni lililotengenezwa kwa spinachi amefanya maonyesho huko Nairobi, Kenya katika kampeni ya kushawishi Wakenya kuacha kula nyama.

Michelle Odhiambo, anayejulikana kama ''The Lettuce Lady" ni kutoka shirika linalotetea haki za wanyama. Amesema kampeni yake ina malengo mawili.

Kwanza nguo yake inahimiza watu kula mboga za majani na pili kuhimiza watu kutokula chama ya kuchoma maarufu sana nchini Kenya kama ''nyama choma''.

Bi Odhiambo,ambaye aliacha kula nyama miaka minane iliyopita amesema chakula ambacho hutumiwa kulisha wanyama wanaochinjwa kinaweza kutumiwa kulisha watu wengi.

Huku akibeba bango lililoandikwa "Let Vegetarianism Grow On You" aliambia watu waliojitokeza kumuona kuwa pia ana wasiwasi kuhusu jinsi wakulima hushugulikia mifugo.

''Mifugo wanafungiwa katika maeneo madogo sana, wanawahasi, wanawachinja na haya yote wanafanya bila kuwapa dawa za kudhibiti uchungu. Hiyo ni haki kweli?''

Bi Odhiambo pia ametoa wito kwa migahawa kubadilisha mapishi na kushugulikia zaidi watu wasiopendelea kula nyama.

Mwandishi wa BBC mjini Nairobi anasema kupika chakula bila nyama, hasa katika maeneo ya mijini ni jambo linalohusishwa na umaskini nchini Kenya.

''Sasa tutakula nini tusipokula nyama? '', aliuliza Mohamed Asman, kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambako kuna jamii ya wafugaji na nyama ndiyo chakula chao cha kila siku.

Kocha mpya kijana kumsaidia Capello


Meneja wa timu ya England, Fabio Capello, amekubali kuteua kocha kijana ambaye ni mzawa wa England ajumuike na Stuart Pearce kwenye kikosi chake cha ufundi, BBC Sport imefahamishwa.

Mkurugenzi wa maendeleo wa chama cha soka cha England, Sir Trevor Brooking, amesema atasaidia kuteua kocha huyo na kuwasilisha mapendekezo yake ifikapo mwezi Disemba.

Pearce, ambaye pia ndiye kocha wa timu ya England ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 21, tayari yumo katika kikosi cha makocha cha Capello.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya bodi ya FA kukutana kujadili ufanisi mbovu wa timu ya England kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.
Nafasi kwa vijana

Mwandishi wa maswala ya michezo wa BBC, Dan Roan alisema: "FA inataka Brooking na Capello kutafuta kocha mwingine kijana kusaidia katika kikosi cha ufundi cha timu ya taifa ya England, bega kwa bega na Stuart Pearce.

Wawili hao watawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na mpango wa kuendeleza wachezaji wa kimataifa na mafunzo ya makocha, huku chama cha soka, FA, kikiwa na shauriku ya kujifunza kutokana na England iliyokuwa ikimwagiwa sifa, kushinda mechi moja tu.

Capello, ambaye aliendelea na kazi yake baada ya mashindano, alisema ataelekeza zaidi nguvu zake kuendeleza wachezaji vijana. Hatua za kwanza zitaanza kuonekana wakati England itakapocheza na Hungaru katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Wembley, tarehe 11 Agosti.

Mabomu Yaua 64 Wakiangalia Kombe la Dunia Uganda


Watu 64 akiwemo Mmarekani mmoja wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Uganda kutokana na mabomu mawili yaliyolipuka sehemu mbili tofauti ambazo mamia ya watu walijazana kuangalia fainali ya kombe la dunia kati ya Hispania na Uholanzi.
Zaidi ya watu 64 wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti ya milipuko ya mabomu mjini Kampala katika maeneo ambayo mamia ya watu walijazana kuangalia fainali ya kombe la dunia.

Raia mmoja wa Marekani ni miongoni mwa watu waliouawa na mabomu hayo. Hadi sasa polisi wamethibitisha vifo vya watu 23 vilivyotokea katika mgahawa wa Kiethiopia na klabu ya rugby.

Mabomu hayo yalilipuka katika sehemu mbili tofauti yakipishana muda kwa dakika 10.

"Taarifa tulizo nazo zinaonyesha kuwa watu 13 wamefariki katika mgahawa wa Ethiopian Village na wengine wengi wamejeruhiwa vibaya huku watu wengine 10 wamefariki katika klabu ya rugby", alisema inspekta wa polisi, Kale Kayihura.

Polisi wamesema kuwa watu wengi wamejeruhiwa vibaya katika matukio hayo mawili ambayo yalitokea huku mamia ya watu wakiwa wamejazana kuangalia mechi ya fainali ya kombe la dunia kati ya Uholanzi na Hispania ambapo Hispania ilitawazwa mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0.

"Mabomu yalilipuka wakati kumbi za baa zikiwa zimefurika watu waliokuwa wakiangalia mechi ya fainali ya kombe la dunia", alisema msemaji wa polisi, Judith Nabakooba.

Kundi la wanamgambo wa Somalia la Al-Shabbab ndilo linalohisiwa kufanya shambulizi hilo kutokana na ahadi waliyoitoa miaka michache iliyopita kuwa watafanya mashambulizi nchini Uganda na Burundi kwakuwa nchi hizo zimepeleka majeshi yake nchini Somalia kuisaidia serikali iliyopo madarakani.

Jumla ya wanajeshi 5000 toka Uganda na Burundi wapo mjini Mogadishu ili kuilinda serikali iliyopo madarakani.

Mtoto Aliyezua Gumzo Kwenye YouTube


Akiwa amevalishwa nepi na mama yake, mtoto huyo anacheza samba katika staili mbalimbali juu ya meza.

Video hiyo yenye urefu wa dakika 2:54 imeishawavutia zaidi ya watu 500,000 tangu ilipowekwa kwenye YouTube wiki hii

Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza


Nyota wa R&B wa Marekani, Chris Brown ambaye alikuwa afanye shoo tatu nchini Uingereza kuanzia kesho, amenyimwa viza ya kuingia Uingereza.

Sababu iliyopelekea anyimwe viza ni kosa lake la kumshushia kipigo na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani, Rihanna mnamo mwezi februari mwaka jana. Brown alihukumiwa kifungo cha nje pamoja na kuamriwa aitumikie jamii kwa kufagia na kukata majani.

Brown alikuwa afanye shoo zake kwenye miji ya London, Birmingham na Glasgow.

Brown aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa amenyimwa viza ya Uingereza lakini ujumbe huo uliondolewa baada ya muda mfupi.

Taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza ilisema kuwa wanayo haki ya kumnyima viza mtu yoyote aliyepatikana na hatia ya makosa makubwa ya jinai. Usalama wa jamii ndio unaopewa kipaumbele.

Watu walionunua tiketi za shoo za Chris Brown wametakiwa na mapromota wa shoo hizo SJM, kuzihifadhi tiketi zao kwani huenda shoo hizo zikafanyika siku yoyote Chris Brown atakapopatiwa viza ya kuingia Uingereza.

50 Cent Choka Mbaya, Ukimuona Huwezi Kumtambua


Picha mpya za mwanamuziki milionea wa Marekani 50 Cent zimetolewa na kuwafanya watu wabaki midomo wazi kwa jinsi ambavyo imekuwa vigumu kumtambua kwa jinsi alivyopungua kilo 25 ndani ya wiki tisa.

50 Cent amejikondesha kwa kunywa maji na juice pekee ili aweze kuigiza kwenye filamu mpya ambayo jikoni ambayo inamuelezea nyota wa mpira wa miguu ambaye anaugua ugonjwa wa kansa.

50 Cent ambaye ana umri wa miaka 34 amekonda sana na amepungua uzito wake toka kilo 97 hadi kilo 72.

50 Cent amejikondesha ili kuleta uhalisia wa mgonjwa wa kansa katika filamu ya "Things Fall Apart", filamu hiyo 50 Cent ndiye nyota wa filamu na prodyuza msaidizi.

Wakati picha mpya za 50 Cent zilipowekwa kwenye mitandao jana watu wengi waligoma kuamini na kusema kwamba picha hizo ni uzushi tu wa kwenye mitandao.

Lakini 50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson alijitokeza na kuthibitisha kuwa picha hizo ni za kweli.

50 Cent alisema kuwa baada ya kumaliza kuigiza kwenye filamu hiyo ataanza kula kama kawaida kurudisha mwili wake wa zamani.

Mwarabu Kuiwakilisha Marekani Mashindano ya Urembo ya Dunia

Rima Fakih Mmarekani mwenye asili ya Lebanon amekuwa Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kushinda mashindano ya Miss USA katika historia ya mashindano hayo.

Katika mashindano yaliyofanyika mjini Las Vegas na kuonyeshwa live na televisheni ya NBC, Fakih aliwafunika jumla ya warembo 50 toka majimbo mbalimbali ya Marekani na kutwaa taji la Miss USA 2010.



Fakih mwenye umri wa miaka 24, alitwaa taji la urembo wa Marekani akifuatiwa na Miss Oklahoma aliyeshika nafasi ya pili, Miss Virginia, Miss Colorado na Miss Maine.

Fakih ataiwakilisha Marekani kwenye mashindano ya urembo ya Miss Universe yatakayofanyika baadae mwaka huu

Burudani Time - Angalia Mkuki Usikuchome


ahazi wanasema:

Malipo ni duniani, akhera kuhesabiwa
usijigeuze nyani, kucheka uliyoombewa,
wajua unakotoka, hujui unakokwenda
mithili ya rabuka, haijui mwanamwenda
hata uwe unaruka, kwa mola huwezi kwenda
-
Alopewa mitihani, mungu hajamuonea
Msikae vikaoni, vidole kumnyooshea

--
Kibwagizo
-----------

Wasafirishe wapeleke pwani na jahazi
Mwanamke nyonga, makalio ni majaliwa

Mrembo wa Temeke Apatikana


Fainali za mashindano hayo ziliwashirikisha jumla ya warembo kumi na mbili.

Mkurugenzi wa Shindano hilo katika Wilaya ya Temeke Ben Kisaka alisema kuwa kutokana na maandalizi mazuri walivyofanya wana uhakika kuwa mwaka huu Miss Tanzania atatoka katika wilaya hiyo.

Katika shindano hilo kivutio kikubwa kilikuwa ni kwa baba na mwana Banana Zorro na Zahiri Zorro ambao wote walikuwa kivutio kikubwa pale walipoimba pamoja jukwaani.

Mshindi wa pili katika shindano hilo alikuwa ni Anna Daudi na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Britney Urassa nafasi ya nne ilikwenda kwa Domitria Innocent na watano alikuwa Ritta Samuel.

Washiriki wote watashiriki katika kambi ya Miss Tanzania ambayo itaanza hivi karibuni baada ya kumalizika kwa mashindno ya umiss ya mikoa na kanda.

Ukimwi na Ushoga Ndani ya Radio Clouds ?


Msanii mkongwe hapa nchini Joseph Mbilinyi aka Mr 11 Sugu, ameliteka jiji la Dar kutokana na albamu yake ya Anti Virus ambayo ndani yake amewapaka live watangazaji na viongozi wa redio ya Clouds FM.

KWa mujibu wa Mr II watangazaji hao wanadaiwa kutumia redio hiyo kwa kuwatongoza wanawake wanaokwenda pale kuomba kazi pia kuzibania kazi za wasanii ambao hawapo katika listi yao.

Mr II pia amewachana live kundi la THT Kituo cha kukuza vipaji Tanzania Kuwa kituo hicho kinatumika kinyume na ilivyotarajiwa.

Albamu hiyo ya Sugu ina nyimbo zaidi ya 14 lakini hapa nchini haziwezi kupigwa katika vituo vya redio kutokana na kujaa matusi ya hadharani, hivyo albamu hiyo imekuwa ikiuzwa chini kwa chini na watanzania wengi wamekuwa wakiishambulia kwa kuinunua hasa wale wapenda mapinduzi katika fani hiyo ya muziki wa kisasa kwani vijana wengi wamekuwa wakibaniwa kazi zao kutokana na kutofahamika au kutokana na kutokuwa na uhusiano muzuri na watu wa redio na Tv.

Majuzi Sugu alikamtwa na polisi na kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano, lakini baadaye aliachiwa kwa dhamana.

MR II amewaweka njia panda watangazaji wa Clouds hasa kwa kuwataja live baadhi ya watangazaji kuwa wanasambaza Ukimwi kwa makusudi huku wakijua kuwa wao ni waathirika wa ugonjwa huo.

Pia aliwataja baadhi watangazaji kuwa ni wasenge jambo ambalo limewafanya watu wengi wajiulize imekuwaje hadi Mr II ameamua kutunga nyimbo hiyo na kuisambaza kwa watanzania?.

"Hapa kuna jambo ambalo kiuhakika litakuja kujulikana siku zijazo kwanini nyimbo hizo zitungiwe tu watangazaji wa Clouds, huku vyombo lukuki vikiwa vipo na havikutajwa hata kimoja?", alisema mmoja wa wadau wa muziki wa Bongo Fleva aliyehojiwa na Nifahamishe kuhusiana na albamu hiyo ya Sugu.

Angalia video ya wimbo huo chini.

Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani


Akipanda jukwaani kufanya shoo yake ya kwanza kubwa baada ya kuingia matatani kwa kumpiga mpenzi wake zamani, Rihanna, Chris Brown aliangua kilio jukwaani wakati akiimba nyimbo ya Michael Jackson.

Brown alipanda jukwaani kufanya shoo ya kumuenzi Michael Jackson wakati wa tamasha la kutoa tuzo za muziki za Black Entertainment Television.

Brown alianza kwa kuwachengua watazamaji kwa shoo ya dansi akiigiza staili mbalimbali za Michael Jackson.

Alipoanza kuimba wimbo wa Michael Jackson "Man In The Mirror" uliotamba sana mwaka 1988, Chris Brown alianza kuangua kilio jukwaani na kushindwa kuendelea kuimba hali iliyopelekea watu waliohudhuria shoo hiyo kuungana naye kuimba nyimbo hiyo.

Pamoja na hisia alizozionyesha jukwaani kuhusiana na kifo cha Michael Jackson, Chris Brown amekumbwa na tuhuma kuwa alizuga kujiliza jukwaani ili watu waanze kumsapoti tena baada ya kashfa ya kumpiga Rihanna mwaka jana.

Chris Brown kutokana na kumpiga Rihanna alipoteza washabiki wengi na baadhi ya wadhamini wake na alihukumiwa kufanya kazi za kuitumikia jamii kwa miezi sita.

Maoni mengi katika tovuti ya MTV.com yalimponda Chris Brown kwa kuonyesha hisia za uongo ili kupata huruma za watu.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kama hisia za Chris Brown zilikuwa za kweli au la