Friday, July 23, 2010

O'Neil yuko tayari kumwuuza Milner


Meneja wa Club ya Aston Villa Martin O'Neill anasema yuko tayari kumuuza mcheza kiungo wake James Milner baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia yake ya kuihama club hiyo.

Tayari Man City ilijaribu kuleta pauni milioni 20 zilizokataliwa na Aston Villa.

Kocha wa Aston Villa amesema mchezaji huyo aliyepewa muda zaidi wa kupumzika kufuatia kushiriki michuano ya Kombe la Dunia atarejea hivi karibuni na labda Man City watarudi na kitita kikubwa zaidi.

Wakati huo huo kampuni ijulikanayo kama EA Sports, maarufu kwa mpangop wake wa 'Fifa Soccer', imeafikiana na ligi ya Premiership kama mshirika wake katika teknolojia ya michezo.

Hata hivyo takwimu kuhusu gharama na fedha zinazohusika hazikutajwa, ingawa EA Sports itapewa haki zaidi katika mipango ya ligi kuu ya England.

Miongoni mwa kazi zinazotarajiwa na kampuni hiyo ni matangazo ya kampuni hiyo kwa mechi zote zitakazotangzwa moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kupitia vituo vya kibiashara kama Sky Sports, ESPN na vingine vya kimataifa.

Pamoja na hayo kampuni hiyo itatoa takwimu za timu bora ya wiki kwenye wavuti yake ya Ligi ya Premier ya England.

No comments:

Post a Comment