Tuesday, July 20, 2010

Chris Brown Adaiwa Kujiliza Jukwaani


Akipanda jukwaani kufanya shoo yake ya kwanza kubwa baada ya kuingia matatani kwa kumpiga mpenzi wake zamani, Rihanna, Chris Brown aliangua kilio jukwaani wakati akiimba nyimbo ya Michael Jackson.

Brown alipanda jukwaani kufanya shoo ya kumuenzi Michael Jackson wakati wa tamasha la kutoa tuzo za muziki za Black Entertainment Television.

Brown alianza kwa kuwachengua watazamaji kwa shoo ya dansi akiigiza staili mbalimbali za Michael Jackson.

Alipoanza kuimba wimbo wa Michael Jackson "Man In The Mirror" uliotamba sana mwaka 1988, Chris Brown alianza kuangua kilio jukwaani na kushindwa kuendelea kuimba hali iliyopelekea watu waliohudhuria shoo hiyo kuungana naye kuimba nyimbo hiyo.

Pamoja na hisia alizozionyesha jukwaani kuhusiana na kifo cha Michael Jackson, Chris Brown amekumbwa na tuhuma kuwa alizuga kujiliza jukwaani ili watu waanze kumsapoti tena baada ya kashfa ya kumpiga Rihanna mwaka jana.

Chris Brown kutokana na kumpiga Rihanna alipoteza washabiki wengi na baadhi ya wadhamini wake na alihukumiwa kufanya kazi za kuitumikia jamii kwa miezi sita.

Maoni mengi katika tovuti ya MTV.com yalimponda Chris Brown kwa kuonyesha hisia za uongo ili kupata huruma za watu.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kama hisia za Chris Brown zilikuwa za kweli au la

No comments:

Post a Comment