Tuesday, July 20, 2010

Chris Brown Anyimwa Viza ya Uingereza


Nyota wa R&B wa Marekani, Chris Brown ambaye alikuwa afanye shoo tatu nchini Uingereza kuanzia kesho, amenyimwa viza ya kuingia Uingereza.

Sababu iliyopelekea anyimwe viza ni kosa lake la kumshushia kipigo na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani, Rihanna mnamo mwezi februari mwaka jana. Brown alihukumiwa kifungo cha nje pamoja na kuamriwa aitumikie jamii kwa kufagia na kukata majani.

Brown alikuwa afanye shoo zake kwenye miji ya London, Birmingham na Glasgow.

Brown aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa amenyimwa viza ya Uingereza lakini ujumbe huo uliondolewa baada ya muda mfupi.

Taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza ilisema kuwa wanayo haki ya kumnyima viza mtu yoyote aliyepatikana na hatia ya makosa makubwa ya jinai. Usalama wa jamii ndio unaopewa kipaumbele.

Watu walionunua tiketi za shoo za Chris Brown wametakiwa na mapromota wa shoo hizo SJM, kuzihifadhi tiketi zao kwani huenda shoo hizo zikafanyika siku yoyote Chris Brown atakapopatiwa viza ya kuingia Uingereza.

No comments:

Post a Comment