Tuesday, July 20, 2010

Mwanamuziki Aliyejiua Kutofanyiwa Sala za Maombi Kanisani


Mwanamuziki nyota wa Romania ambaye alijiua mwenyewe kwa kunywa sumu ya wadudu hatasaliwa misa kamili ya mazishi kutokana na kanisa la orthodox la nchini humo kusema kuwa amefanya dhambi kubwa kwa kujiua.
Kanisa la orthodox la nchini Romania limegoma kumfanyia misa kamili ya mazishi nyota wa muziki wa nchini humo kwakuwa alijiua mwenyewe.

Nyota wa muziki mwanamke Madalina Manole alijiua mwenyewe kwa kunywa sumu kali ya wadudu siku ya jumatano ambayo pia ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na kutimiza umri wa miaka 43.

Mwili wa Manole uligunduliwa na mume wake wakati huo Manole alikuwa tayari ameishaiaga dunia baada ya kunywa sumu.

Kanisa la orthodox limesema kuwa mchungaji mmoja atafanya misa fupi sana kwaajili ya Madalina Manole ambayo itafanyika katika maeneo ya nje ya kanisa.

Kanisa hilo linaamini kuwa mtu kujiua ni dhambi kubwa sana.

Manole atazikwa siku ya ijumaa katika mji wake wa Ploiesti kaskazini mwa jiji la Bucharest.

Manole alikuwa maarufu sana kwa miziki ya country akitamba zaidi kwa mashairi yake ya mapenzi. Kifo chake kimewashtua watu wengi sana nchini Romania

No comments:

Post a Comment