Monday, August 30, 2010
Chelsea yazidi kuongoza England
Didier Drogba
Didier Drogba
Chelsea vinara wa Ligi Kuu ya England wameendeleza rekodi ya ushindi kwa msimu huu baada ya kuwalaza Stoke City mabao 2-0.
Pamoja na ushindi huo Chelsea walikosa kufunga mkwaju wa penalti baada ya Frank Lampard aliyecheza chini ya kiwango kupiga shuti hafifu lililodakwa na mlinda mlango Thomas Sorensen wa Stoke City.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Florent Malouda kipindi cha kwanza na bao la pili lilipachikwa na Didier Drogba kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo Chelsea wamefikisha pointi tisa kwa michezo mitatu na wanaongoza ligi hiyo.
Katika pambano lililochezwa mchana, Arsenal nao waliweza kujiongezea pointi tatu baada ya kuwafunga Blackburn Rovers nyumbani kwao mabao 2-1 na kufikisha ponti saba.
Matokeo mengine kwa michezo ya leo ya Ligi Kuu ya England, Blackpool walitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Fulham, Tottenham walikubali kipigo cha bao moja nyumbani kwao dhidi ya Wigan na Wolves walikwenda sare ya bao 1-1 walipowakaribisha Newcastle
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment