Jaribio la dereva asiyeona kuweka rekodi ya kuendesha gari kwa kasi zaidi halikufanikiwa nchini Uingereza.
Mike Newman aliendesha gari yake kwa maelekezo kupitia redio ambayo hutolewa na mwongozaji aliye juu kwenye helikopta, akijaribu kufikia rekodi ya dunia.
Lakini matumaini yake yalitoweka wakati gari yake maalum yenye uwezo wa kufikia kasi ya kilometa 416, Keating KTR ilipoharibika. Alitumia gari ya akiba aina ya Nissan GTR ingawa haikuweza kufua dafu kuvunja rekodi, kwa sasa rekodi ya mtu asiyeona ni kilometa 292 kwa saa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment