Thursday, August 12, 2010

David Beckham atoswa na Capello


Kila lenye mwanzo huwa na mwisho wake, David Beckham, wakati wa kilele cha uhodari wa kusakata kabumbu alikuwa kivutio kikubwa kila mahali alipokwenda.

Lakini sasa kocha Fabio Capello aliyelaumiwa kwa kuwa na timu yenye wachezaji wazee kwenye Kombe la Dunia, ameamua kuanza na mkongwe Beckham, kumwambia ondoka upishe chipukizi kwa kuwa umri umevuka mpaka unaotakiwa. Katika taarifa hii, Zuhura Yunus anasimulia mwisho huo wa Beckham kuiwakilisha England kimataifa.

No comments:

Post a Comment