Friday, August 13, 2010

Wenger kutia saini mkataba

Wakati msimu mpya wa ligi kuu ya England ya Premier unapoanza, meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema muda mfupi ujao atatia saini makubaliano ya kuendelea kubaki katika uwanja wa Imarati.

Mfaransa huyo, mwenye umri wa miaka sitini, na ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika, amesema mkataba mpya utaonyesha ana imani na timu.
Arsenal, chini ya uongozi wa Wenger, imepata ushindi katika michuano 11, katika kipindi cha miaka 13, lakini tangu kombe la FA mwaka 2005, haijapata chochote.
Arsenal itaanza msimu mpya siku ya Jumapili, kwa kucheza ugenini dhidi ya Liverpool, ikiongozwa na meneja mpya Roy Hodgson.

"Lazima nithibitishe imani yangu kwa kuonyesha jitihada zangu," alisema Wenger.

Arsenal mara ya mwisho kupata ushindi wa ligi ya Premier ilikuwa mwaka 2004.
Wenger alijiunga na Arsenal mwezi Septemba, mwaka 1996, na kufanya mabadiliko makubwa katika timu.






Walishinda ligi ya mwaka 1998, 2002, na 2004, Kombe la FA mwaka 1998, 2002, 2003 na 2005, na kisha kufika fainali za klabu bingwa na pia Kombe la UEFA.

No comments:

Post a Comment