Kirk Bauer, Neil Duncan na Dan Nevins
Maaskari watatu wa zamani raia wa Marekani waliokatwa viungo vyao vya mwili wamepanda mlima Kilimanjaro, wakistahamili maporomoko na majeraha kufikia kilele cha mlima mrefu barani Afrika kila mmoja akiwa na mguu mmoja tu ambao ni imara.
Watu hao kutoka Vietnam, Afghanistan na Iraq, walikwea hadi kufikia juu ya mlima huo wenye urefu wa mita 5,891 uliopo nchini Tanzania.
Iliwachukua siku sita kufikia kileleni kwa nia ya kuonyesha kuwa ulemavu haumaanishi huna uwezo wa kufanya lolote.
Safari hiyo huchukua siku tano hadi sita, na ilibidi watu hao kusimama mara kwa mara ili kurekebisha miguu yao ya bandia, baada ya kuteleza sana.
Wakweaji hao wa mlima ni Dan Nevins, mwenye umri wa miaka 37, ambaye alipoteza miguu yake nchini Iraq, Neil Duncan, wa miaka 26, alipoteza miguu yote miwili katika shambulio la bomu lililotegwa barabarani Afghanistan mwaka 2005; na Kirk Bauer, mwenye miaka 62, aliyepoteza mguu mmoja huko Vietnam mwaka 1969.
Bw Bauer aliliambia shirika la habari la AP, " Ikiwa watu watatu waliokatwa viungo kutoka vita vitatu tofauti na kutoka vizazi tofauti na wana mguu mmoja tu wanaweza kupanda mlima Kilimanjaro, marafiki zetu wengine walemavu wanaweza kutoka na kupanda mlima au kuendesha basikeli au kuogelea, na wanaweza kuwa na maisha yenye afya njema."
Bw Nevis alipata jeraha katika kigutu ya moja ya miguu yake hiyo ya bandia na baada ya kufika kileleni aliondoshwa kwa kutumia machela.
Bw Bauer ni mkurugenzi mtendaji wa michezo ya walemavu wa Marekani, shirika lililopo mjini Wasington DC linaloshughulika na uzima wa afya na ushiriki wa michezo kwa walio na ulemavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment