Thursday, August 26, 2010

Redknapp asema haogopi timu yoyote


Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amesema wapo tayari kukabiliana na timu yoyote katika hatua ya makundi kuwania Ubingwa wa Ulaya.

Spurs iliilaza Young Boys mabao 4-0 pambano lililochezwa uwanja wa White Hart Lane na kufanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 1961-62.

Kuna kila dalili Tottenham wakapangwa kundi moja na mabingwa watetezi Inter Milan ama Barcelona, lakini Redknapp amejigamba hawahofii timu yoyote.

Amesema"Tupo tayari kukabiliana na yeyote, tumekwishafuzu hatua ya makundi tutapambana na yeyote bila kuogopa".

Mabao matatu yaliyofungwa Peter Crouch na moja la Jermain Defoe, yaliiwezesha Tottenham kulipa deni la kufungwa mabao 3-2 ugenini katika mechi ya awali na hivyo kuingia hatua hiyo kwa jumla ya mabao 6-3 dhidi ya timu ya Bern kutoka Switzerland.

No comments:

Post a Comment