Monday, August 30, 2010

Mascherano avutiwa na Barcelona









Liverpool imemuuza mcheza kiungo Javier Mascherano aliyepania kujiunga na klabu ya Uhispania Barcelona kwa takriban pauni milioni 17.25 imefahamishwa BBC.
Javier Mascherano

Mascherano sasa kuichezea Barcelona

Hata hivyo mpango mzima wa usajili utategemea mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina kufanikiwa majaribio ya afya huko Barcelona.

Klabu ya Barcelona imethibitisha kwenye tovuti yao kwamba vilabu vimeafikiana juu ya usajili wa Mascherano kwa kipindi cha misimu minne ijayo.

Pindi majaribio yakifanikiwa Barcelona itawafahamisha wakuu wa Liverpool na hivyo kukamilisha usajili.

Taarifa ya Barcelona imeongezea kusema kuwa mpango mzima wa usajili ulikamilishwa baada ya juhudi zilizofanywa na klabu katika dakika za mwisho ambapo mchezaji mwenyewe alishiriki majadiliano.

Inatazamiwa kuwa Mascherano atawasili huko Barcelona mwishoni mwa juma hili.

Katika mpango mzima Liverpool ilitaka irudishe pauni milioni 18 ilizolipa kumsajili mchezaji huyo alipowasili kutoka klabu ya West Ham.

Kabla ya hapo Liverpool ilikataa malipo ya pauni milioni 16 zilizopendekezwa na Barcelona siku saba zilizopita.

Hata hivyo hakushiriki mechi kati ya Manchester City na Liverepool

No comments:

Post a Comment