Friday, August 6, 2010
Torres kubaki Liverpool
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania na pia klabu ya Liverpool Fernando Torres amekomesha tetesi za muda mrefu kwamba huenda akasajiliwa na club ya Chelsea au Manchester City kwa kutangaza wazi kwamba ataichezea klabu yake ya Liverpool msimu unaoaza mwezi huu.
Fernando Torres
Tangu mwisho wa msimu uliopita Liverpool ilipomaliza katika nafasi ya saba na Kocha Rafael Benitez kutimuliwa Fernando Torres amekuwa gumzo la kuweza kuhamia katika vilabu vingine, kama vile Manchester City na Chelsea.
Fernando Torres
Lakini kuwasili kwa kocha mpya Roy Hodgson pamoja na nahodha Steven Gerrard kubaini kuwa ataiongoza klabu hiyo kama nahodha kumempa moyo mshambuliaji huyo kurudi katika klabu yake kwa imani kuwa wanaweza kutimiza ndoto na hamu ya mashabiki kwa kushinda ubingwa wa Ligi kuu ya Premiership.
Torres amesema, ''kweli nimefurahi kurudi , nina furaha kuwaona tena marafiki zangu.''
"Msimamo wangu kwa mashabiki na klabu yangu ni ule ule kama siku ya kwanza nilipotia saini kuichezea klabu hii na natazamia kukabiliana na changamoto za Ligi kuu." amesema Torres.
Torres 'El Nino'
Liverpool ambayo inatazamiwa kuuzwa, hadi sasa imemsajili mcheza kiungo Joe Cole kutoka Chelsea huku Chelsea ikimchukua Yossi Benayoun, wakati kiungo mwingine Javier Mascherano ameonyesha kutaka kuondoka klabu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment