Angela Scognamiglio mwenye umri wa miaka 33 alichaguliwa kuwa mrembo mpya mnene wa Italia katika mashindano ya urembo yanayojulikana kama "Miss Chubby".
"Nimefurahishwa sana, najihisi kama nimeshinda bahati nasibu", alisema Angela baada ya kuvalishwa taji lake la mrembo mnene wa Italia mbele ya watu 2500 waliojitokeza kushuhudia mashindano hayo ya urembo yaliyofanyika kwenye mji wa Forcoli.
Angela alitwaa taji hilo baada ya kuwafunika warembo wenzake 30 waliokuwa wakiliwania taji hilo.
Sharti kubwa la kushiriki mashindano hayo ni kwa mwanamke kuwa na uzito zaidi ya kilo 100.
Warembo walipita mbele ya watu wakiwa wamevalia mavazi mbalimbali kuanzia nguo za kulalia mpaka nguo za kuogelea.
Lakini tukio muhimu la mashindano hayo lilikuwa ni la kupima uzito ambapo warembo walipita juu ya mzani mkubwa huku uzito wao ukionekana kwenye luninga. Mrembo mwenye uzito mkubwa ndiye aliyekuwa mshindi.
Hakuna zawadi kubwa kwa mshindi zaidi ya keki kubwa ambayo mshindi alishea na jamaa zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment